4 Mei 2016 - 18:47
Mpaka sasa Madaesh wameangamia wangapi?

Waziri wa ulinzi nchini Uingereza ametangaza idadi ya waliokufa wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria na Iraq

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: waziri wa ulinzi wa Uingereza siku ya Jumatano ametoa idadi ya magaidi waliokufa ambao ni wanachama wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria, Iraq na kaskazini mwa Afrika .
Msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza akitoa ujumbe wake katika mkutano aliofanya na waandishi wa habari ametangaza idadi ya magaidi wa kikundi cha Daesh waliokufa  nchini Syria na Iraq kufikia magaidi elfu mbili na mia tano.
Aidha waziri wa ulinzi wa Uingereza: ametoa idadi ya watu waliokufa kufuatia mashambulio yaliofanya na umoja wa kusambaratisha kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq na Syria, pia katika mashambulizi ya kuzuia kuenea mashambulizi ya kigaidi katika sehemu zingine duniani hususan maeneo ya kaskazini mwa Afrika.
Naye ametangaza kuwa idadi ya magaidi hao waliokufa kwa kiasi fulani imepungua kwa kipindi cha miaka miwili, huku akisisitiza kuwa serikali ya Uingereza ilikuwa kipaumbele katika mapambano dhidi ya kikundi hicho katika maeneo mbalimbali.
Takwimu iliotolewa haijaweka wazi kuwa magaidi hao 25000 waliokufa kutoka kikundi cha kigaidi cha Daesh wameuliwa kupitia majeshi ya Iraq, Syria, majeshi ya Urusi au majeshi ya Hizbulla? Au  wanajumuishwa na waliokufa kupitia majeshi ya umoja wa kupambana na ugaidi.
mwisho wa Habari/290